Description
Watu wengi sana wana mtazamo wa maombi usiotokana na Neno la Mungu ila matukio mbalimbali kwenye filamu, maelezo ya watu waliosema wametoka kuzimu, wachawi walioamua kuokoka, habari za kuambiwa, mambo ya kutunga, kuangalia watu WANAVYOFANYA hata kama mambo hayo yote yanafanyika kinyume na Neno la Mungu. Maombi ni fundisho kamili kwenye Biblia wala haipaswi kufanywa kwa kupapasapapasa.
Katika kitabu hiki tutajifunza angalau mambo ya msingi kuhusu maombi kwa kutumia uchambuzi wa maandiko matakatifu. Baadhi ya mambo tutakayojifunza katika kitabu hki ni kama ifuatavyo:
- Maombi ni nini?
- Nani anatakiwa kuomba?
- Tunamwomba nani?
- Kwanini tuombe?
- Tunaomba nini?
- Tunaomba wakati gani?
- tunaomba mara ngapi?
- Mungu anajibuje?
- Majibu yanapokelewaje?
Na mengine mengi…
Reviews
There are no reviews yet.