Description
MWONGOZO WA AWALI WA KUKUSAIDIA KUSOMA NA KUELEWA MAANDIKO MATAKATIFU.
Chimbuko lolote la udhaifu wa tafsiri ya maandiko ni matokeo ya kutotaka kujifunza kwa umakini. Kwa muda mchache ambao nimehubiri kwa kutumia Biblia nimegundua ya kwamba habari nyingi tulizonazohatujui hata zimeandikwa wapi. Mambo mengi tuliyofundishwa ni yale ambayo tulimsikia mhubiri akisema, na sisi tukawaambia wengine nao wakawaambia wengine hata kama hatujui amefikaje kwenye tafsiri hiyo.
Ukweli ni kwamba ukianza kusoma kwa utulivu kuna vitu hutokuja kuvisema tena. Bali utahakiki kama ndivyo mambo yalivyo kama watu wa Beroya kwenye Matendo ya Mitume 17:11. Kitabu hiki kitakupa mwongozo wa awali wa namna ya kusoma na kuchambua maandiko matakatifu na hatimaye kupata yale ambayo yamekusudiwa yalipoandikwa.
Reviews
There are no reviews yet.